Netanyahu kwa muda mrefu amekuwa akishinikiza kutokomezwa kwa Hamas huko Gaza, lakini alisema katika taarifa,” Madai kwamba tumekubali sitisho la mapigano bila masharti sio sahihi.”
Biden alielezea mpango mpya wa sitisho la mapigano huko Gaza wiki iliyopita ambao unajumuisha kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Hata kama maafisa wa Israel wametilia mashaka yaliomo katika pendekezo hilo la kusitisha mapigano, jeshi limetangaza kwamba mateka wengine wanne waliotekwa nyara na Hamas sasa wamethibitishwa kuwa wamekufa, wakiwemo wazee tatu walioomba bila mafanikio watekaji wao wa Hamas kuwaachilia.
Maafisa wa Marekani wanasema wanaamini ikiwa Hamas itakubaliana na pendekezo hilo la kusitisha mapigano, jambo ambalo bado haijafanya, basi Israel itakubali pia.
Msemaji wa serikali ya Israel alisema kwamba “vita vitasitishwa kwa masharti ya kuwaachilia mateka” baada ya hapo mazungumzo yataendelea juu ya jinsi ya kufikia lengo la vita vya kuitokomeza Hamas.
Forum