Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:16

Ndugu wawili wafanya biashara wazaliwa wa India wanaotuhumiwa ufisadi nchini Afrika Kusini, wakamatwa Dubai


Atul Gupta kutoka familia ya Gupta, akionekana nje ya mahakama mjini Johannesburg, June 11, 2021. Picha ya AP
Atul Gupta kutoka familia ya Gupta, akionekana nje ya mahakama mjini Johannesburg, June 11, 2021. Picha ya AP

Ndugu wawili wafanya biashara wazaliwa wa India ambao wanadaiwa kuwa mstari wa mbele kwenye mtandao mkubwa wa ufisadi nchini Afrika Kusini wamekamatwa huko Dubai, Pretoria imetangaza Jumatatu.

Kukamatwa kwao kunajiri wakati uchunguzi ukikamilishwa kuhusu uporaji mkubwa wa taasisi za serikali wakati wa enzi za rais wa zamani Jacob Zuma.

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini “imethibitisha kwamba ilipata taarifa kutoka kwa mamlaka za kisheria katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwamba watoro hao wa sheria, ambao ni Rajesh na Atul Gupta walikamatwa,” wizara hiyo imethibitisha katika taarifa.

Walishtumiwa kutoa hongo na badala yake kupewa kandarasi kubwa za serikali na zenye faida kubwa na kuwa na ushawishi kwenye uteuzi wa mawaziri.

Kukamatwa kwao kunajiri mwaka mmoja baada ya polisi ya kimataifa Interpol kutoa tahadhari ya kuwasaka mwezi Julai mwaka jana.

“Majadiliano kati ya mamlaka mbalimbali za kisheria huko UAE na nchini Afrika Kusini kuhusu kitakachofuata yanaendelea,” imesema wizara ya sheria ya Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG