Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:14

Nchi zilizosaini mkataba na Iran zaahidi kuuendeleza


Amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump wa Marekani akitangaza nia yake ya kujiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran Jumanne, May 9, 2018.
Amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump wa Marekani akitangaza nia yake ya kujiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran Jumanne, May 9, 2018.

Kufuatia uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kujiondoa katika mkataba wa kimataifa unaohusu programu ya nyuklia ya Iran, nchi nyingine zilizosaini mkataba huo zimesema Jumatano kwamba wao wataendelea kuheshimu makubaliano hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian ameiambia radio RTL kwamba mkataba huo “haujakufa.” Amesema Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Iran Hassan Rouhani watafanya mazungumzo Jumatano, na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Ujerumani watazungumzia hali hiyo na maafisa wa Iran Jumatatu.

Pamoja na juhudi hizo za kidiplomasia, mawaziri wa mambo ya nje wa Russia na Ujerumani watafanya mazungumzo yao Alhamisi huko Moscow na suala la Iran likiwa katika ajenda.

Waziri wa mambo ya nje wa China ameahidi kutetea makubaliano ya 2015 kama yalivyofikiwa katika mkataba wa kimataifa juu ya mpango wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia (JCPOA)
na amesema kuwa inasikitishwa na uamuzi wa Trump kujiondoa katika mkataba huo.

Tamko la pamoja lililotolewa kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya limesema kuwa mkataba wa JCPOA mpaka sasa umeonyesha mafanikio katika kufikia malengo yake ya kuhakikisha kuwa Iran haitengenezi silaha za nyuklia, na kuondoshwa kwa vikwazo dhidi ya Iran kumekuwa na athari chanya kwenye biashara na mahusiano.

Hilo linakinzana kabisa na maoni ya Trump kwamba kile alichokisema Jumanne kuwa “mkataba huo ni mbaya na umeegemea upande moja ambao haukutakiwa kamwe kabisa kufikiwa.”

Katika kauli yake kutoka chumba cha diplomasia cha White House, Rais huyo alitangaza kuwa Marekani inarejesha vikwazo vyote vinavyohusiana na nyuklia ambavyo vilisitishwa kama ni sehemu ya mkataba wa JCPOA.

Amesema kuwa mkataba huo, uliofikiwa chini ya Rais mstaafu Barack Obama, “haukuleta utulivu, haukuleta amani, na hautoweza kufanya hivyo kabisa.”

Ndani ya Bunge la Iran Jumatano, uamuzi wa Trump ulipokelewa na wabunge kwa kuchoma moto kipande cha karatasi kilichokuwa na picha ya bendera ya Marekani na kipande kingine kilichokuwa ni mfano wa mkataba wa nyuklia.

Spika wa Bunge Ali Larijani amesema Idara ya nyuklia ya Iran ijitayarishe kuendeleza shughuli zote zilizokuwa zimesimama.

Na Rais Rouhani mapema alisema Iran itaendelea kuheshimu mkataba huo wa kimataifa.

XS
SM
MD
LG