Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:16

Narendra Modi kutembelea Russia Jumatatu


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ( kushoto) akisalimiana na Rais wa Russia Vladimir Putin. Picha ya maktaba. Sept. 16, 2022.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ( kushoto) akisalimiana na Rais wa Russia Vladimir Putin. Picha ya maktaba. Sept. 16, 2022.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi anaelekea Russia Jumatatu kwa ziara ya siku mbili, ili kuimarisha ushirikiano, wakati Moscow ikiwa na uhusiano wa karibu sana na China ambayo ni hasimu mkubwa wa India.

Wachambuzi wa New Delhi wanasema mkutano kati ya Modi na Rais wa Russia Vladimir Putin, Jumanne utaondoa dhana kwamba India imelegeza uhusiano wake wa karibu na Russia ambaye ni mshirika wake wa muda mrefu, wakati pia ikendelea kuimarisha ushirikiano wake na Marekani.

Kikao hicho kitakuwa cha kwanza tangu Russia ilipoivamia Ukraine, wakati India ikiwa haiungi mkono upande wowote tangu wakati huo. Kufikia sasa India haijakosoa vita hivyo, wala kuungana na mataifa ya Magharibi katika kuiwekea Moscow vikwazo.

Ingawa viongozi wa India na Russia wamekuwa wakifanya vikao vya kila mwaka tangu 2000, hakuna vikao vilivyofanyika tangu Putin alipoitembelea New Delhi 2021. Licha ya kupanua wigo wa kununua silaha katika miaka ya karibuni, India kwa kiasi kikubwa inategemea silaha kutoka Russia.

Takriban theluthi moja ya vifaa vya ulinzi vya India ni kutoka Moscow, ikilinganishwa na theluthi mbili miaka mitano iliyopita.

Forum

XS
SM
MD
LG