Netumbo Nandi Ndaitwah ni naibu waziri mkuu katika serikali ya sasa, na uteuzi wake katika nafasi ya juu ya chama cha Swapo, umefanyika wakati wa kongamano kuu la chama.
Kulingana na katiba ya chama cha SWAPO, Nandi Ndaitwah atakuwa mgombea wake wa urais wakati rais wa sasa Hage Geingob atakapomaliza mihula yake miwili madarakani, ambayo imesalia miezi 15.
Ndaitwah amewashinda wagombea wengine wawili akiwemo waziri mkuu wa sasa katika uchaguzi uliohusisha wanachama wa ngazi ya juu 700 na kuhudhuriwa pia na viongozi wa chama kinachotawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF.