Naibu gavana wa zamani wa benki kuu ya China, Fan Yifei, amehukumiwa kifo kwa kuchukua rushwa na kupewa ahueni ya miaka miwili, vyombo vya habari vya serikali vimesema Alhamisi, wakati kukiwa na msukumo mkubwa wa kupambana na rushwa katika sekta ya fedha.
Fan alikutwa na hatia ya kukubali mali kinyume cha sheria yenye thamani ya karibu dola milioni 54.55, akitumia nafasi zake za juu katika benki kuu na taasisi nyingine za kifedha, ikiwemo China Construction Bank, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ikinukuu mahakama ya China.
Kufuatia kupewa ahueni ya miaka miwili, hukumu ya kifo ya Fan itabadilishwa na kuwa kifungo cha maisha, hakuna uwezekano wa kupewa msamaha, shirika la habari la serikali lilinukuu “Huanggang Intermediate People’s Court”, katika jimbo la Hubei.
Fan Yifei alipokea rushwa ya kiasi kikubwa sana, mazingira ya uhalifu wake yalikuwa mabaya sana, athari za kijamii zilikuwa mbaya sana, na maslahi ya serikali na watu walipata hasara kubwa sana, mahakama ilinukuliwa ikisema hivyo.
Forum