Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 28, 2024 Local time: 09:00

Mzozo wa kidiplomasia watokota kati ya Niger na Benin


Wafanyakazi wa China na Niger wakiwa kwenye ujenzi wa bomba la mafuta . Oktoba. 10. 2022. Picha ya maktaba.
Wafanyakazi wa China na Niger wakiwa kwenye ujenzi wa bomba la mafuta . Oktoba. 10. 2022. Picha ya maktaba.

Mradi wa bomba la mafuta linalojengwa na China nchini Niger, na ambalo lina uwezo wa kufanya taifa hilo kuwa muuzaji mkubwa wa mafuta kwenye mataifa ya nje una hatari ya kusitishiwa kutokana na mzozo wa ndani wa kiusalama, pamoja na wa kidiplomasia na taifa jirani la Benin.

Mizozo yote miwili ni kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliofanyika Niger mwaka uliopita na kuondoa madarakani serikali iliochaguliwa kidemokrasia. Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,930 linaanzia kwenye kinu cha mafuta cha Agadem, kilichotengenezwa na China, hadi kwenye bandari ya Cotonou, nchini Benin.

Mradi huo unalenga kuongeza maradufu uzalishaji wa mafuta wa Niger, na ulitiwa saini kati ya China na shirika la kitaifa la mafuta, kwa gharama ya dola milioni 400. Hata hivyo bomba hilo lililazimika kufungwa wiki iliopita kutokana na mzozo wa kidiplomasia na Benin.

Pia wiki hii lilishambuliwa na waasi wa Liberation Front, huku likitishia kuendelea na mashambulizi, iwapo mkataba huo kati ya serikali na China hautafutwa. Kundi hilo linaloongozwa na aliyekuwa kiongozi wa waasi Salah Mahmoud, lilichukua silaha baada ya mapinduzi ya kijeshi, hali inatotishia usalama wa taifa, ambao tayari unayumba yumba.

Wachambuzi wanasema kuwa hali huyo huenda ikaathiri pakubwa, Niger, moja wapo ya mataifa masikini duniani, na ambalo hutegemea misaada ya kigeni, ambao sasa hivi imesitishwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliofanywa.

Forum

XS
SM
MD
LG