Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:12

Mzozo wa bomba la mafuta kati ya Sudan kusini na Sudan waongezeka


Eneo la mabomba ya mafuta huko Sudan Kusini.
Eneo la mabomba ya mafuta huko Sudan Kusini.

Mzozo wa bomba la mafuta kati ya Sudan kusini na Sudan waongezeka baada ya mazungumzo ya siku sita.

Sudan Kusini imetishia kufunga kabisa bomba la mafuta linalopitia bahari ya sham, baada ya mazungumzo ya kutanzua mgogoro baina yake na Sudan kushindikana katika duru nyingine ya mazungumzo Jumatano juu ya mgawo wa mapato ya mafuta baina ya nchi hizo mbili. Majadiliano ya siku sita yanayodhaminiwa na Umoja wa Afrika yalimalizika Jumatano huku pande zote mbili zikionekana kugawanyika zaidi ya ilivyokuwa wakati mazungumzo hayo yalipoanza. Mwakilishi wa Sudan Kusini katika mazungumzo hayo Pagan AMum aliwaambia waandishi habari baada ya majadiliano ya muda mrefu Jumanne usiku kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuzungumzia malipo ya mafuta na serikali ya Khartoum. Mzozo huu umejikita katika swala la kiasi cha fedha Sudan Kusini inatakiwa kulipa Sudan kwa kutumia bomba la mafuta linalobeba mafuta kutoka upande wa Kusini kupitia bandari ya Sudan kwenye bahari ya Sham. Afisa mwingine wa Sudan Kusini anasema mafuta yaliyoibwa na Sudan tangu mzozo baina ya nchi hizi mbili uanze ni ya thamani ya takriban dola bilioni moja. Amum amesema Sudan kusini imeapa kufunga bomba hilo la mafuta hadi pale Sudan itakapokubali kulipa fedha zote za mafuta yaliyoibwa. Anaongeza kuwa Sudan Kusini itaendelea na mpango wa kujenga bomba lingine la mafuta ambalo halitapita upande wa Kaskazini.

XS
SM
MD
LG