Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 06, 2025 Local time: 15:35

Mzaliwa wa Kenya aapishwa kuwa Seneta Australia


Seneta Gichuhi akiapishwa kwenye bunge la Australia
Seneta Gichuhi akiapishwa kwenye bunge la Australia

Mwanamke mmoja mzaliwa wa Kenya, aliapishwa Jumanne kama seneta wa Australia, wiki tatu baada ya Mahakama ya juu nchini humo kuidhinisha uchaguzi wake.

Lucy Gichuhi, amekuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika, kuwa seneta kwenye bunge la nchi hiyo.

Gichuhi atawakilisha moja ya majimbo kumi na mawili ya Kusini mwa Australia. Mwanasiasa huyo amechukua nafasi yake Bob Day, ambaye uchaguzi wake ulibatilishwa na mahakama, baada ya kupatikana kwamba ulikuwa umegubikwa na dosari.

Soma pia taarifa inayowiana: Mzaliwa wa Kenya ashinda kiti cha Seneta Australia

Gichuhi, mwenye umri wa miaka 54, aliwania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha Family First, lakini chama hicho kikajiunga na vyama vingine vya Kikonsevativu.

Alihamia Australia mnamo mwaka wa 1999. Uamuzi wa mahakama ya juu nchini humo, ulisitisha maswali yaliyoibuka kuhusu uraia wake.

Gichuhi alichukua uraia wa Australia mnamo mwaka wa 2001. Amekuwa mmoja wa maseneta 76 wa Australia.

XS
SM
MD
LG