Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:08

Myanmar: Jeshi limeongeza hali ya dharura, uchaguzi kuchelewa


Jeshi la Myanmar April 17 2019
Jeshi la Myanmar April 17 2019

Utawala wa kijeshi wa Myanmar umeongeza muda wa hali ya dharura kwa miezi sita, hatua inayochelewesha uchaguzi mpya kama ilivyoahidiwa, wakati unapambana na upinzani.

Nchi hiyo ya Asia Kusini Mashariki imekuwa katika mgogoro tangu mapinduzi ya Februari 2021 yalimaliza miaka kumi ya majaribio ya kidemokrasia na kupelekea maandamano makubwa, na msako mkali dhidi ya uasi.

Miaka mitatu na nusu baadaye, utawala wa kijeshi unakumbana na wakati mgumu kukabiliana na upinzani wenye silaha, na umepoteza udhibiti wa sehemu kadhaa za nchi kwa muungano wa makundi ya kijamii ya walio wachache.

Utawala huo umeshindwa kuandaa uchaguzi mpya kama ilivyokuwa umepangwa baada ya hali ya dharura ya miaka miwili kwa kile kimetajwa kama kuwepo vitendo vya kigaidi kutoka kwa wapinzani wake.

Mkuu wa utawala wa kijeshi Min Aung Hlaing, amependekeza kuongezwa muda huo akisema iutoa nafasi ya kuandaa uchaguzi wa haki na huenda uchaguzi sasa ukaandaliwa mwaka 2025.

Forum

XS
SM
MD
LG