Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 11:42

Mwili wa raia wa Tanzania aliyekufa akipigania mamluki wa Russia nchini Ukraine kuzikwa Tanzania


Wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner la nchini Russia
Wapiganaji wa kundi la mamluki la Wagner la nchini Russia

Serikali ya Tanzania imethibitisha kutokea kwa kifo cha mtanznaia Nemes Tarimo kilichotokea akipigania Russia nchini Ukraine.

Tarimo anasemekana kujiunga na kundi la mamluki la Wagner la Russia wakati alipokuwa anazuiliwa gerezani kwa kifungo cha miaka saba kutokana na makosa ya kupatikana na dawa za kulevya.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Dkt Stergomena Tax amesema kwamba wizara hiyo kwa kushirikiana na serikali ya Russia imeratibu kusafirishwa kwa mwili wa mtanzania huyo aliyefariki dunia Oktoba 24, 2022 kwa ajili ya kupelekwa Tanzania kwa majishi.

“Wizara imeendelea kuwasiliana na serikali ya Russia kuhakikisha kwamba mwili wa marehemu unarejeshwa nchini Tanania, unakabidhiwa kwa familia yake na taratibu za mazishi zifanyike kulingana na taratibu na mila zetu na desturi zetu za Tanzania,” amesema Tax akiongezea kwamba “mwili umeondoka Russia asubuhi hii na tunatarajia utafika wakati wowote kuanzia sasa.”

Hata hivyo Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imesisitiza kwamba watanzania wanapaswa kufahamu sheria za nchi ya kwamba hakuna mtanzania anayeruhusiwa kujiunga na jeshi la nchi nyingine akiongezea kwamba raia wa Tanzania wanaoishi katika nchi zingine wanstahili kufuata sheria na taratibu za nchi wanazoishi.

Nemes Tarimo alienda Russia kwa ajili ya masomo ya juu mwaka 2020.

Alikuwa akisoma shahada ya uzamili katika katika masomo ya biashara katika chuo kikuu cha Moscow.

Alikamatwa na kuhukumiwa miaka 7 gerezani mwezi march mwaka 2022 baada ya kupatikana na dawa za kulevya.

Inaaminikwa kwamba alishawishiwa kujiunga na kundi la mamluki la Wagner kwa ahadi kwamba atasamehewa makosa yake na kuachiwa huru.

XS
SM
MD
LG