Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC anafanya uchunguzi wa dharura kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mji wa al-Fashir huko Darfur ambao umekuwa uwanja mpya wa mapambano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF.
Katika taarifa ya video iliyotolewa leo Jumanne, mwendesha mashtaka Karim Khan alisema ICC inafanya uchunguzi wa kina kuhusu uhalifu wa kinyama unaowezekana kufanywa hivi sasa huko Darfur.
"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu shutuma za kusambaa uhalifu wa kimataifa unaofanywa huko al-Fashir na maeneo yanayoizunguka, kama tunavyozungumza," Khan alisema, akiongeza kuwa ofisi yake inachunguza tuhuma hizo kwa uharaka.
Wachunguzi wake wameona kuna shutuma za kuaminika kwa kile kilichoonekana kama mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia, ubakaji mkubwa na mashambulizi dhidi ya hospitali, aliongeza.
Forum