Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:33

Mwendesha mashitaka maalum Jack Smith alipata hati ya siri ya upekuzi wa Twitter ya Trump


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na mwendesha mashitaka Maalum Jack Smith
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na mwendesha mashitaka Maalum Jack Smith

Jaji aliipiga faini ya dola 350,000 kampuni ya Twitter kwa kukosa kutekeleza upesi amri hiyo

Mwendesha mashitaka maalum wa wizara ya sheria ya Marekani Jack Smith alipata hati ya siri ya upekuzi Januari mwaka jana kwa taarifa kutoka kwenye akaunti ya Twitter ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump rekodi za mahakama zilionyesha siku ya Jumatano. Jaji aliipiga faini ya dola 350,000 kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii kwa kukosa kutotekeleza upesi amri hiyo.

Trump alitumia takriban muhula wake wote wa miaka minne katika Ikulu ya Marekani akiandika maelfu ya maoni kwenye Twitter ingawa haikuwa wazi ni habari gani hasa Smith alikuwa akitafuta kutokana na hati hiyo.dsw

Maoni hayo ya Twitter yalikuwa hadharani tayari huku Trump mara nyingi akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii kuwakashifu wapinzani wake wa kisiasa na wengine ambao asiokubaliana nao. Pia aliwaarifu wafuasi wake kuhusu mikutano ya kisiasa kama ule wa karibu na White House wa Januari 6, 2021 kabla ya ghasia katika bunge la Marekani zilizoandaliwa na wafuasi wake kujaribu kuwazuia wabunge kuidhinisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Forum

XS
SM
MD
LG