Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:59

Mwandishi wa habari wa  Al Jazeera auwawa alipokuwa akiripoti uvamizi wa Israel


Waombolezaji wakiwa wamezunguka jeneza la Shireen Abu na Al Jazeera wanasema ripota wao aliuwawa na vikosi vya Israel huko ukingo wa magharibi.
Waombolezaji wakiwa wamezunguka jeneza la Shireen Abu na Al Jazeera wanasema ripota wao aliuwawa na vikosi vya Israel huko ukingo wa magharibi.

Mwandishi wa habari wa  Al Jazeera alipigwa risasi na kuuawa alipokuwa akiripoti uvamizi wa Israel katika mji unaokaliwa kimabavu huko Ukingo wa Magharibi Jumatano.

Mtangazaji na mwanahabari mwingine ambaye aliyejeruhiwa katika tukio hilo alivilaumu vikosi vya Israel, huku Israel ikisema kuna ushahidi kwamba wawili hao walipigwa risasi na Wapalestina.

Shireen Abu Akleh, mwanahabari maarufu wa Kipalestina wa idhaa ya lugha ya Kiarabu ambaye pia ni raia wa Marekani, alipigwa risasi na kufariki dunia muda mfupi baadaye Ali Samoudi, mwandishi mwingine wa habari wa Palestina, alilazwa hospitali akiwa katika hali nzuri baada ya kupigwa risasi mgongoni.

Mtandao huo wenye makao yake nchini Qatar ulikatisha matangazo yake na kutangaza kifo chake. Katika taarifa iliyopeperushwa kwenye idhaa yake, ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulaani na kuviwajibisha vikosi vya Israel .

XS
SM
MD
LG