Kesi ya mwandishi wa habari wa Zimbabwe anayeshutumiwa kuwasaidia waandishi wa habari wawili wa New York Times kuingia nchini kinyume cha sheria imeanza tena Jumatatu.
Jeffery Moyo mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa ajili ya uchapishaji wa Marekani amekanusha kwamba aliwasaidia waandishi hao kupata vitambulisho bandia.
Waandishi hao, Joao Silva na Christina Goldbaum walirejeshwa Afrika Kusini siku kadhaa baada ya kuwasili kwao.
Moyo alikamatwa mwezi Mei mwaka 2021 na kesi yake kuanza kisikilizwa Januari.
Kama atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.
Mashahidi zaidi katika kesi hiyo watasikilizwa wakati kesi inaanza tena katika mji wa kusini wa Bulawayo.
Moyo alisema alihojiwa na kitengo cha polisi wa kupambana na ugaidi na alikamatwa na kufungwa jela bila dhamana kwa wiki tatu.
Mwandishi huyo amesema anaamini yuko mahakamani kwa kazi yake ya uandishi wa habari.