Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:13

Mwanasheria mkuu wa Marekani ajiuzulu


Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr ajiuzulu.
Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr ajiuzulu.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr, mmoja wa washirika wakubwa wa Rais Donald Trump, anajiuzulu wakati kukiwa na mvutano wa muda mrefu na rais juu ya madai yasio na msingi ya rais ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika na uchunguzi juu ya mtoto wa rais mteule Joe Biden.

Barr alikwenda siku ya Jumatatu White House, ambapo Trump alisema mwanasheria mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Trump ameonyesha hasira yake hadharani juu ya taarifa ya Barr aliyoitoa kwa shirika la habari la Associated Press mapema mwezi huu kwamba Idara ya Sheria haikuona udanganyifu mkubwa wa uchaguzi ambao ungebadilisha matokeo ya uchaguzi huo.

Trump anasema Naibu Mwanasheria Mkuu Jeff Rosen atakuwa Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG