Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:09

Mwanariadha wa Kenya aadhibiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu


Wanariadha wa Kenya wakifanya mazoezi magharibi mwa Kenya, picha ya AP.
Wanariadha wa Kenya wakifanya mazoezi magharibi mwa Kenya, picha ya AP.

Kitengo cha maadili cha riadha kimemsimamisha mwanariadha wa Kenya wa mbio ndefu (Marathon) Mark Kangogo kwa madai ya kukiuka kanuni za kutumia dawa za kuongeza nguvu. Ni mwanariadha wa nne kutoka Kenya kuadhibiwa na kitengo hicho.

Kitengo hicho (AIU) kimesema katika taarifa kwamba Kangogo amesimamishwa kwa muda baada ya vipimo kuonyesha kuwa ndani ya mfumo wake wa damu kulionekana dawa mbili zilizopigwa marufuku, Norandrosterone na Triamcinolone acetonide.

Kusimamishwa kwa Kangogo ni kashfa ya karibuni ambayo kwa mara nyingine inatishia kuharibu sifa za riadha ya Kenya.

Kufikia mwaka huu, wanariadha wa Kenya 21, wengi wao wakiwa wale wa mbio ndefu, wamekwisha adhibiwa kwa madai ya kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Jumatatu, mwanariadha mwenzake wa mbio za marathon Philemon Kacheran amepigwa marufuku kutoshiriki mashindano kwa miaka mitatu na kitengo hicho cha maadili, baada ya kuonekana kuwa na viwango vya juu vya testosterone.

XS
SM
MD
LG