Mkuu wa taasisi ya uchaguzi ya kitaifa amesema kwamba hesabu hiyo inaonyesha kwamba Sheinbaum, ambaye ni meya wa zamani wa mji wa Mexico, anaelekea kupata ushindi wa kati ya asilimia 58.3 na 60.7 ya kura zilizopigwa.
Mshindani wake mkuu, Xochitl Galvez, ambaye ni seneta kutoka vyama vya upinzani na mfanyabiashara, ana kati ya asilimia 26.6 na 28.6.
Mgombea wa mrengi wa kati Jorge Alvarez Maynez ana kati ya asilimia 9.9 na 10.8.
Hesabu pia inaonyesha kwamba chama chake Sheinbaum kinaelekea kupata idadi kubwa ya viti katika baraza la Congress.
Forum