Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 13:02

Mwanaharakati wa mazingira nchini Uganda ameachiliwa huru


Ramani ya Uganda na nchi zilizo karibu na taifa hilo.
Ramani ya Uganda na nchi zilizo karibu na taifa hilo.

Stephen Kwikiriza alipatikana Jumapili jioni akiwa ametupwa kando ya barabara huko Kyenjojo

Mwanaharakati wa mazingira nchini Uganda ambaye alipinga mradi mkubwa wa mafuta unaoongozwa na kampuni kubwa ya Ufaransa ya TotalEnergies ameachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa siku tano, mwajiri wake amesema Jumatatu.

Stephen Kwikiriza alipatikana Jumapili jioni akiwa ametupwa kando ya barabara huko Kyenjojo, umbali wa saa tano magharibi mwa mji mkuu Kampala, alisema Samuel Okulony, mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala wa Mazingira.

Mwanaharakati huyo alisema alipigwa na maafisa wa jeshi, Okulony alisema kwenye ujumbe wa shirika la habari la AFP, akiongeza kwamba alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Kampala. “Kwikiriza yuko hai, sasa yuko salama, na anaungana tena na familia yake. Hali yake sio nzuri baada ya kupigwa, na kunyanyaswa kwa wiki nzima”.

Maafisa waandamizi wa jeshi la Uganda hawakujibu mara moja maombi ya AFP ya kuwataka watoe maoni yao. Okulony alipongeza shinikizo la kimataifa kufuatia kuachiliwa kwa Kwikiriza.

Forum

XS
SM
MD
LG