Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:07

Mwanahabari wa Pakistan auwawa Nairobi


Mwandishi wa habari wa Pakistan Arshad Sharif Dec. 15, 2016.
Mwandishi wa habari wa Pakistan Arshad Sharif Dec. 15, 2016.

Polisi wa Kenya pamoja na jamaa za mmoja wa wanahabari mashuhuri kutoka Pakistan Arshad Sharif mwenye umri wa miaka 50, wamedhibitisha kuuwawa kwake kutokana na kile kimetajwa kama kupigwa risasi kwa makosa na polisi.

Sharif ambaye ni mwanahabari wa uchunguzi amepigwa risasi kichwani Jumapili usiku baada ya dereva wake kukaidi amri ya kusimama kwenye kizuizi cha polisi katika barabara kuu kuelekea Nairobi kutoka mji wa Magadi, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa kwenye mojawapo wa magazeti mashuhuri nchini humo.

Mwanahabari huyo mwenye wafuasi milioni 2 kwenye mtandao wake wa Twitter alitoroka Pakistan Agosti kwa madai ya kutishiwa maisha , pamoja na kesi kadhaa mahakamani dhidi yake akiwa na wanahabari wengine, kwa tuhuma za uchochezi dhidi ya utawala. Kabla ya kuondoka nchini Pakistan, Sharif aliendesha kipindi maarufu cha kisiasa cha Power Play kwenye televisheni maarufu ya ARY.

Taarifa za kifo chake zimeenea kwa haraka kote Pakistan, wengi wakitoa rambi rambi zao pamoja na kukemea tukio hilo. Polisi wa Kenya wamesema kuwa uchunguzi unaendelea kutokana na tukio hilo.

XS
SM
MD
LG