Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:47

Mwanahabari wa Eritrea aliyefungwa jela apewa tuzo ya Sweden ya Edelstam


Maanadamano ya awali ya kuitisha kuachiliwa kwa mwanahabari Dawit Isaak aliefungwa jela Eritrea tangu 2001.
Maanadamano ya awali ya kuitisha kuachiliwa kwa mwanahabari Dawit Isaak aliefungwa jela Eritrea tangu 2001.

Mwanahabari wa Sweden mwenye asili ya Eritrea ambaye amekuwa kizuizini Eritrea bila mawasiliano kwa zaidi ya miaka 23 Jumatatu amepewa tuzo ya Sweden ya Haki za binadamu kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya kijieleza, jopo la tuzo hiyo limesema.

Dawit Isaak alikuwa miongoni wa kundi la takriban watu darzeni 2 wakiwemo mawaziri na wabunge pamoja na wanahabari, waliokamatwa kwenye msako wa Septemba 2001. Isaak sasa amepewa tuzo ya Edelstam kutokana na mchango wake wa kupigania haki za kujieleza, Imani na kulindwa kwa haki za binadamu, taasisi ya Edelstam imesema kupitia taarifa.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kuwa Isaak ni mfungwa kwa kihisia wakati kundi la Wanahabari wasio na Mipaka, RSF, likisema kuwa Isaak pamoja na wenzake waliofungwa ndiyo wanahabari waliozuiliwa kwa muda mrefu zaidi ulimwenguni.

Wataalam wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishinikiza Asmara kumuachilia mara moja. Eritrea haijakuwa ikitoa taarifa kumhusu, na kuna hofu kwamba huenda hayupo hai tena, na iwapo yu hai basi ana umri wa miaka 60.

Forum

XS
SM
MD
LG