Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 14:36

Muungano wa wafanyakazi wa usafiri wa anga Kenya watishia mgomo


Shirika la ndege la Kenya-Kenya Airways
Shirika la ndege la Kenya-Kenya Airways

Mgomo huenda ukasababisha usumbufu kwa Kenya Airways na kwa shughuli za uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta

Muungano wa wafanyakazi wa usafiri wa anga Kenya umesema Jumatatu kuwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Kenya Airways na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya wataanza mgomo kuanzia Agosti 19 mwaka huu kufuatia pendekezo la uwekezaji kutoka kampuni ya India ya Adani Airport Holdings, kwenye uwanja mkuu wa ndege nchini humo.

Mgomo huo huenda ukasababisha usumbufu mkubwa kwa Shirika la ndege la Kenya Airways na kwa shughuli za uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, kitovu muhimu cha usafiri barani Afrika.

"Tutafikiria tena azma yetu ya kushiriki katika hatua ya viwanda, ikiwa tu mkataba wa Adani Airport Holdings Limited, unaachwa kabisa", alisema Moss Ndiema, Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi wa Anga Kenya.

Mwezi uliopita Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya ilisema kuwa pendekezo la uwekezaji kutoka Adani Airport Holdings ilijumuisha njia ya pili ya kuondokea ndege kwenye wanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Forum

XS
SM
MD
LG