Kiongozi huyo wa Uganda akihutubia mkutano wa wajumbe kutoka jopo la wajumbe wa matifa yanayoshughulikia suala la Somalia, alisema ikiwa uchaguzi wa bunge na rais utafanyika kama ulivyopangwa na Umoja wa Matiafa kabla ya mwisho wa mwaka huu basi wanaharakati wa Al Shabab watatumia muda huo kushamnbulia na kuvuruga utaratibu wote.
Hata hivyo mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somali, Balozi Augustine Mahiga amesisitiza haja ya kufanyika kwa uchaguzi kwa haraka na kuishutumu serikali ya mpito kwa kutoweza kutekeleza ahadi na majukumu yake yaliyopangwa miaka miwili iliyopita.
Akizungumza na sauti ya amerika huko Kampala Bw Mahiga alisema ni lazima kuendelea kuwahimiza viongozi wa Somalia kusikilizana na kuendelea na utaratibu wa kudumisha amani na uthabiti nchini mwao.