Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:06

Museveni ahutubia UN na kuunga mkono maudhui ya mwaka huu


President Yoweri Museveni addresses the UN General Assembly on September 20, 2016.
President Yoweri Museveni addresses the UN General Assembly on September 20, 2016.

Na BMJ MURIITHI

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, alihutubia mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne na kusema kuwa anafurahia sana maudhui ya mwaka huu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na kubadili maisha.

Museveni alisema mada hiyo imejiri wakati mwafaka kwani sehemu ndogo tu ya dunia, hususan katika nchi za Magharibi, zinafurahia utajiri ilhali maeneo mengi duniani, ikiwemo nchi ya Uganda, yanaathirika na umaskini.

Aidha alisema watu maskini duniani kote wamejikamkamua, na kwamba bara la Afrika lina watu takribani milioni 414 walioondokana na umaskini.

"Mnamo mwaka wa 2004, asilimia 56 ya raia wa Uganda walikuwa wanaishi katika umaskini, lakini hivi sasa idadi hiyo ni asilimia 19 na nina matumaini kuwa ifikapo mwaka 2017 itafikia asilimia 10. Na je dunia sasa ni bora zaidi kwa huu utajiri huu mpya unaonufaisha karibu ulimwengu mzima," alisema.

Rais huyo ni mmoja wa viongozi wa nchi na serikali kutoka barani Afrika na kwingineko ulimwenguni wanaowakilisha mataifa yao kwenye Kongamano la mwaka huu.

"Tuna furaha kuwa hatimaye, ajenda ya dunia hivi sasa inagusa maswala ambayo ni muhimu katika kuleta mabadiliko kwa jamii zilizochochea mapinduzi ya viwanda, hususan kujumuishwa kwa nishati katika orodha ya SDG, ni tofauti na ajenda ya zamani," aliongeza Museveni.

Kikao cha Jumatano kinatarajiwa kuhutubiwa na viongozi wa Zimbabwe, Ghana, Togo na Libya, kati ya wengine.

Marais wa Kenya na Tanzania walituma wawakilishi wao kwa mkutano wa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG