Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:16

Mugabe atazikwa mjini Harare Jumapili - Familia


Jeneza lililobeba mwili wa Rais wa zamani wa Zimabwe, Robert Mugabe.
Jeneza lililobeba mwili wa Rais wa zamani wa Zimabwe, Robert Mugabe.

Mwanzilishi wa taifa la Zimbabwe Robert Mugabe atazikwa katika makaburi ya kitaifa mjini Harare Jumapili hii. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa familia aliyezungumza Ijumaa huku maelezo yake yakitofautiana na yale  yaliotolewa siku moja kabla.

Wafuasi wa Mugabe walipanga foleni kuutazama mwili wake Alhamisi katika uwanja wa mpira wa Rufaro mjini Harare.

Mke wa Mugabe, Grace, pamoja na wanafamilia wengine waliongoza waombolezaji kuuaga mwili.

Tangu alipofariki mwishoni mwa wiki jana, mvutano uliibuka kati ya familia na serikali kuhusu ni wapi ambapo angezikwa.

Ingawa Rais Emmerson Mnangagwa alimtaja Mugabe kama baba wa taifa, baadhi ya wanafamilia walihoji ni kwa nini serikali ilitaka azikwe kwenye eneo la kuwazika mashujaa wa kitaifa, na ili hali "viongozi hao hao walimdhririsha kwa kumuondoa mamlakani kwa kutumia jeshi."

Familia ilikuwa ikishikilia kwamba ingependa azikwe kijijini kwake na wala siyo mjini Harare.

Mmoja wa waombolezaji abeba picha ya marehemu Robert Mugabe, 11 septemba 2019.
Mmoja wa waombolezaji abeba picha ya marehemu Robert Mugabe, 11 septemba 2019.

Maelfu ya waombolezaji wakivalia fulana za ZANU PF walikusanyikla katika uwanja huo kutoa heshima zao katika sehemu ambapo Mugabe aliapa kwa mara ya kwanza alipochukua madaraka mwaka 1980.

Mugabe alisimamia uchumi wa taifa hilo lililogubikwa na mfumuko wa bei, madai ya rushwa na upinzani kutoka chama kikubwa cha saisa cha MDC.

Licha ya hayo wazimbabwe wengi bado wanamkumbuka kiongozi huyo wa zamani kama mkombozi wao kutoka kwa utawala wa wazungu wachache waliokuwa wameshikilia ardhi na uwezo wa kupata elimu.

XS
SM
MD
LG