Jack Harlow, Kendrick Lamar na Lil Nas X wanaongoza kwa kuteuliwa mara saba kila mmoja, wakifuatiwa na Doja Cat na Harry Styles wenye sita kila mmoja.
Wasanii wengine waliotajwa mwaka huu ni Billie Eilish, Drake, Dua Lipa, Ed Sheeran, Taylor Swift na The Weeknd.
Mashabiki wanaweza kushiriki na kuwapigia kura nyota wanaowapenda katika maeneo 22 yasioegemea kijinsia, ikijumuisha video ya mwaka, msanii bora wa mwaka, ushirikiano bora na aina mbili mpya: video bora zaidi ya muda mrefu na utendakazi bora zaidi.
VMA za 2022 zitaonyeshwa moja kwa moja kutoka Kituo cha Prudential cha New Jersey siku ya Jumapili, Agosti 28 saa 2 usiku saa za Marekani Mashariki.