Polisi walirusha mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Nairobi, mashirika matano ya kutetea haki, pamoja na Amnesty International na Chama cha Madaktari Kenya, yalisema katika taarifa ya pamoja siku ya Alhamisi.
Kuwepo kwa maganda yaliyotumika kulibainisha kulikuwa na matumizi ya risasi walisema, na kuongeza kuwa zaidi ya waandamanaji 100 wamekamatwa kote nchini Kenya.
Mamlaka huru ya Uangalizi wa Polisi (IPOA) ilisema Ijumaa ilikuwa imeorodhesha taarifa ya kifo cha mwanamume mmoja kinachodaiwa kuwa ni matokeo ya kupigwa risasi na polisi na majeraha kadhaa mabaya waliyopata baadhi ya waandamanaji wakiwemo maafisa wa polisi.
Forum