Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:06

Mtoro wa jela aliyekimbilia Tanzania arejea gerezani Afrika Kusini


Thabo Bester akionekana kwenye camera ya Televisheni katika mahakama kuu ya mjini Cape Town, Afrika Kusini, Mei 3, 2012, katika kesi ya mauaji dhidi yake.
Thabo Bester akionekana kwenye camera ya Televisheni katika mahakama kuu ya mjini Cape Town, Afrika Kusini, Mei 3, 2012, katika kesi ya mauaji dhidi yake.

Mtoro wa jela mbakaji na muuaji ambaye aliacha maiti iliyoungua ndani ya chumba chake cha gereza wakati wa muda wa mapumziko kwa wafungwa, alirejea gerezani nchini Afrika Kusini baada ya kukimbilia nchini Tanzania, maafisa wamesema Alhamisi.

Kesi hiyo iliziaibisha mamlaka na kuzua hasira mpya juu ya uzembe wa polisi wa Afrika Kusini na mfumo wa mahakama ya jinai.

Aliyepewa jina la “mbakaji kwenye Facebook”, Thabo Bester, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa ubakaji, wizi na mauaji mwaka 2012, aliwarubuni waathirika kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kuwabaka na kuwaibia.

Alimua muathirika mmoja.

Alitoroka katika gereza binafsi mjini Bloemfontein mwaka mmoja uliopita, lakini polisi walisema waligundua kuwa alitoroka mwezi uliopita.

Bester alikamatwa Ijumaa iliyopita na polisi wa Tanzania pamoja na mwanamke ambaye inadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye, pamoja na mla njama raia wa Msumbiji.

XS
SM
MD
LG