Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:03

Msongo wa mawazo bado ni tatizo kubwa duniani


Michoro inayoonyesha hali mbali mbali za msongo wa mawazo
Michoro inayoonyesha hali mbali mbali za msongo wa mawazo

Shirika la Afya Duniani Ijumaa limeadhimisha siku ya afya duniani likionya kwamba msongo wa mawazo (depression) ni moja ya sababu kuu za afya mbaya duniani.

Msongo huo ambao unaripotiwa kuwaathiri takriban watu milioni 300 kote duniani. Idara hiyo ya Umoja wa Mataifa imewasihi watu kutafuta tiba kwa msongo wa mawazo, ambao unaweza kupelekea ulemavu na hata kifo.

WHO inasema mzozo, vita na majanga ya asili ndiyo vigezo vikuu kwa mtu kupata msongo wa mawazo.

Idara ya Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa katika kila watu watano kuna mtu mmoja ambaye ameathiriwa na msongo wa mawazo au wasi wasi. Hasa ikizingatiwa kiwango cha tatizo lilivyo, na kusema misaada kwa afya ya akili na kijamii iwe ni sehemu ya misaada ya kibinadamu.

Mbali ya hali hizi, WHO inaripoti kuwa msongo wa mawazo ni sababu inayoongoza katika mtu kupata ulemavu. Mkurugenzi wa WHO katika idara ya afya ya akili na matumizi mabaya ya madawa, Shekhar Saxena anasema msongo wa mawazo ni janga la ulimwengu kwa watu kujiua.

“Duniani kote, watu 800,000 wanafariki kwasababu ya kujiua kila mwaka na hii ni sawa na kifo kimoja kila sekunde 40. Kwahiyo, wakati tunakabiliana na idadi ya vifo, ambavyo kwa hakika ni bahati mbaya katika maeneo yenye mizozo na vita, pia tunahitaji kukumbuka kwamba kuna milipuko ya siri inayoendelea duniani, ambayo huua idadi kubwa ya watu bila ya kutangazwa au kuzungumziwa sawa,” amesema Bwana Saxena.

Saxena ameiambia VOA hakuna tofauti kubwa katika kiwango cha msongo wa mawazo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Ameelezea kwamba watu wengi wenye msongo wa mawazo wanaishi katika nchi za daraja la chini na kati.

“Msongo wa mawazo ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake, asilimia 5.1 dhidi ya asilimia 3.6 miongoni mwa wanaume. Vigezo vingine ni umaskini, ubaguzi, na hali nyingine zote za maisha – iwe ni masuala sugu au ya hapo kwa hapo, hasa miongoni mwa vijana wadogo,” amesema Saxena.

Anasema matibabu kwa kawaida yanahusisha matibabu ya kisaikolojia, dawa za mfadhaiko na mchanganyiko wa dawa hizo. Anasema si muhimu kuwa a mtaalamu wa kutibu msongo wa mawazo. Anasema kinachojulikana tiba na madaktari wa kawaida, wauguzi au wafanyakazi wa afya inaweza kuwa na ufanisi mkubwa.

XS
SM
MD
LG