Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:54

Mshukiwa wa matukio ya milipuko Texas auwawa


Polisi wakilinda eneo ambalo mshukiwa wa milipuko ya mabomu alijilipua huko Austin, Texas, Machi 21, 2018.
Polisi wakilinda eneo ambalo mshukiwa wa milipuko ya mabomu alijilipua huko Austin, Texas, Machi 21, 2018.

Polisi mjini Austin, Texas, wanasema mshukiwa ambaye anahusishwa na mlolongo wa milipuko ya vifurushi vilivyokuwa na mabomu hatari ameuawa baada ya kulipua bomu lililokuwa katika gari yake wakati maafisa wa polisi wanamkaribia kumkamata.

Mkuu wa Polisi Austin Brian Manley amewaambia waandishi wa habari kuwa vyombo vya usalama vilipata uhakika juu ya utambulisho wa mtu huyo kuwa ni mzungu Jumanne jioni na Jumatano alfajiri, na waliweza kugundua gari lake lililokuwa katika hoteli mmoja karibu na Austin kabla hajakimbia na baadae kulipua mabomu hayo.

Manley amesema wachunguzi wanaamini mtu huyo ndiye aliyehusika na mabomu matano yaliyolipuka katika eneo la Austin tangu Machi 2, 2018. Milipuko hiyo iliwauwa watu wawili na kuwajeruhi wanne wengine.

Manley aliongeza kuwa vyombo vya usalama hawafahamu iwapo mshukiwa huyo alikuwa njiani kwenda kupeleka bomu jengine, na hawana uhakika kuwa alikuwa akifanya mashambulizi hayo peke akiwa peke yake.

Manley amesema wachunguzi mpaka sasa hawajajua sababu iliopelekea mtu huyo kufanya mashambulizi hayo.

Afisa mmoja alipata majeraha madogo katika mlipuko wa mapema Jumatano katika barabara kuu, na afisa mwengine alipiga bunduki kuelekea eneo la mlipuko huo.

Rais Donald Trump amevipongeza vyombo vya usalama muda mchache baada ya tukio hilo la kupatikana mshukiwa huyo katika ujumbe wake wa Twitter.

“Mshukiwa wa mlipuko wa mabomu amekufa. Vyombo vya usalama vimefanya kazi nzuri na wote walioshiriki!” amesema Trump.

Shambulizi la mwisho lilitokea Jumanne wakati kifurushi chenye bomu kilipolipuka katika jengo la shirika la Federal Express inayosafirisha vifurushi karibu na mji wa San Antonio, uliopo kilomita 100 kusini magharibi ya Austin. Mfanyakazi mmoja wa shirika hilo alijeruhiwa kidogo.

XS
SM
MD
LG