Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 22:45

Msako, kamatakamata mpya vyaendelea katika uchunguzi London


Watu wakiomboleza waliopoteza maisha katika daraja la London
Watu wakiomboleza waliopoteza maisha katika daraja la London

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema Jumatatu kuwa polisi wamewatambua watu wote watatu waliohusika na shambulizi na kuua watu saba na kujeruhi 50 wengine Jumamosi Jijini London.

May amesema majina yao yatatangazwa “wakati uchunguzi unaoendelea ukiruhusu kufanya hivyo,” na vyombo vya usalama vimekuwa vikiwashikilia watu 11 kuhusiana na uchunguzi huo.

Amesema polisi bado wanashughulikia suala la kuwatambua wale wahanga wa mashambulizi hayo, lakini mpaka sasa inajulikana kuwa waliouawa ni watu wa mataifa kadhaa.

“Haya yalikuwa mashambulizi dhidi ya London na Uingereza, lakini pia ilikuwa ni shambulizi dhidi ya uhuru ulimwenguni ,” amesema.

Polisi London waliendelea kufanya msako zaidi Jumatatu na kuwatia nguvuni “idadi kadhaa” ya watu wakati uchunguzi katika maeneo kadhaa ya Newham na Barking yakiendelea.

Polisi wamesema kuwa shambulizi la Jumamosi lilifanywa na watu watatu waliokuwa ndani ya gari ambalo kwanza liliwagonga watembea kwa miguu katika daraja la London, kisha wakashuka na kuwachoma visu watu wengi katika soko lililokuwa karibu na eneo hilo kabla polisi kuwapiga risasi na kuwaua.

“Tunajaribu kujua iwapo kuna mtu yoyote alikuwa akiwasaidia na kujua historia ya shambulizi hili kwa kadiri ya uwezo wetu,” Mkuu wa kituo cha polisi cha Metropolitan Cressida Dick ameiambia Sky News.

Kikundi cha Islamic State kimedai kuhusika na shambulizi hili kupitia shirika lake la habari Amaq.

XS
SM
MD
LG