Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:11

Alexei Navalny afungwa miaka 15 Russia


 Alexei Navalny
Alexei Navalny

Mahakama moja nchini Russia imemhukumu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny kutumikia kifungo cha miaka 15, siku moja baada ya kiongozi huyo na waandamanaji 100 kukamatwa katika mkutano dhidi ya ufisadi.

Navalny alichukuliwa mpaka mahakama ya Moscow Jumatatu masaa machache kabla ya Kremlin kutangaza kuwa maadamano hayo ni “uchochezi” wa uvunjifu wa amani, na kuwashtumu waandaaji wa mkutano huo kuwa wamewalipa vijana iliwahudhurie.

Mahakama imesema kuwa alikuwa na hatia ya kukaidi amri ya polisi. Kabla ya hapo, alilipishwa faini ya kiwango cha Dola za Marekani 350 kwa kuandaa maandamano kinyume cha sharia.

Maelfu ya waandamanaji Russia katika miji mbali mbali nchini kote Jumapili wakiitikia wito wa Navalny kutaka wale walioko kwenye madaraka wawajibishwe.

OVD-Info, ni taasisi inayo fuatilia ukandamizaji wa kisiasa Russia, wamesema katika tovuti yao kuwa zaidi ya watu 1,000 walikamatwa katika maandamano hayo ya Moscow peke yake.

Hata hivyo idadi hiyo ya waliokamatwa haikuweza kuthibitishwa na vyombo vingine na shirika la habari la serikali TASS limewanukuu askari wa Moscow wakisema kuwa walikuwa wamewakamata watu 500, akiwemo Navalny

XS
SM
MD
LG