Jeshi la Israel limethibitisha tukio hilo na kwamba wote watatu walikuwa wanajeshi na walipatiwa matibabu, huku mmoja akiwa katika hali mbaya.
Mapigano kati ya Waisraeli na Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yameongezeka katika mwaka uliopita.
Kulingana na makadirio ya shirika la habari la Associated Press, takriban Wapalestina 86 wameuawa na wanajeshi wa Israel au kupambana kwa kufyatuliana risasi.
Mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya Waisraeli yamesababisha vifo vya watu 15 katika kipindi hicho.