Hayo uyalijiri huku mshukiwa aliyekamatwa kuhusiana na moto wa awali, akitarajiwa kufikishwa mahakamani.
Moto wa awali, wa siku ya Jumapili ulisababisha paa la jengo jipya ambako wabunge hufanyia vikao vyao, kuporomoka.
Paa la jengo la kale, ambalo lilijengwa mnamo mwaka wa 1884, na ambako ndiko vikao vya baraza kuu la bunge hufanyika, pamoja na vile vya Baraza la Kitaifa la Mikoa, pia liliporomoka.
Bunge lilisema katika taarifa yake kwamba ni malori sita tu kati ya 10 ya zimamoto ambayo sasa yamesalia kwenye eneo la tukio na ilitumainiwa kuwa malori zaidi yangeondolewa baadaye.
Mwanamume mwenye umri wa miaka 49 aliyeshtakiwa kwa uchomaji moto, na makosa mengine ikiwemo wizi, alitarajiwa kufikishwa mahakamani leo Jumanne.