Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 26, 2025 Local time: 12:28

Moto unawaka kwenye mlima mrefu zaidi Afrika wa Kilimanjaro, Tanzania


Moto unaowaka kwenye mlima Kilimanyaro karibu na kambi ya Karanga, nchini Tanzania.
Moto unaowaka kwenye mlima Kilimanyaro karibu na kambi ya Karanga, nchini Tanzania.

Moto mkubwa umetokea kwenye mlima Kilimanjaro karibu na kambi ya Karanga, nchini Tanzania.

Chanzo cha moto huo hakijabainika na juhudi za kuuzima zinaendelea.

Mlima Kilimanjaro, ulio karibu na wilaya ya Moshi, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania, ndio mlima mrefu zaidi Afrika (Futi 19,340) na ni kivutio kikubwa cha watalii kutoka kote duniani. Mlima huo pia ni chemichemi kubwa ya maji.

Kulingana na gazeti la The Citizen, moto huo umeanza kuwaka Ijumaa usiku, Oktoba 21, 2022.

Mkuu wa idara ya hifadhi nchini Tanzania William Mwakilema, amesema kwamba juhudi zinaendelea kuuzima moto huo.

Kanda za video na picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha waelekezi wa watalii wakijaribu kuzima moto huo.

Moto huo unawaka kutoka sehemu za Mweka ukielekea Moorland ambapo nyasi zimekauka.

Mwezi Oktoba, moto uliwaka kwenye mlima Kilimanjaro na kuharibu nyumba za muda za watalii 15, pamoja na mali nyingine ya mamilioni ya pesa.

Karibu watalii 50,000 hukwea mlima Kilimnjaro kila mwaka.

XS
SM
MD
LG