Maafisa walidhani kwamba moto huo ulikuwa umezimwa kabla ya kuendelea kuwaka tena siku ya Jumanne.
Moto huo ulianza ijumaa jioni karibu na kambi ya Karanga, ambapo watalii huanzia safari yao kukwea mlima huo wenye urefu wa futi 13,000.
Upepo mkali unaripotiwa kusababisha moto huo kuanza kuwaka tena.
Karibu watu 400, wakiwemo wanafunzi walikuwa wakipambana na moto huo jumapili na wakaamini kwamba ulikuwa umezimika, kabla ya kuonekana tena katika sehemu nyingine za mlima.
Hatari ya kutokea maafa kutokana na moto unaoteketeza misitu katika sehemu mbali mbali za dunia inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Wanasayansi wameonya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na binadamu yanaendelea kusababisha athari kubwa ikiwemo hali mbaya sana ya hewa, kuongezeka kwa joto duniani na hali mbaya ya ukame.
Moto unaowaka sasa kwenye mlima Kilimanjaro umetokea miaka miwili baada ya kutokea moto mwingine mwezi Oktoba mwaka 2020. Kwenye eneo la kilomita 95 mraba za msitu.