Huku vipimo vya joto vikifikia nyuzi joto 48, za vipimo vya Celcius, katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo la Afrika Kaskazini, nchi hiyo ilirekodi mioto 97 katika mikoa 16, inayosambazwa na upepo mkali, wizara ya mambo ya ndani ilisema.
Mioto hiyo iliua watu 34, wakiwemo wanajeshi 10, wakati ikikumba maeneo ya makazi, wizara ya mambo ya ndani ilisema, ikisahihisha idadi ya awali ya watu 15 waliofariki.
Kulingana na idadi hiyo ya awali, watu 26 pia walijeruhiwa.
Watu 1,500 walihamishwa kutoka mikoa ya Bejaia, Bouira na Jijel mashariki mwa mji mkuu Algiers, kulingana na wizara ya mambo ya ndani.
Mikoa hiyo mitatu katika eneo la pwani ya Mediterranean nchini Algeria imeshuhudia mioto mibaya zaidi.
Rais Abdelmadjid Tebboune jana Jumatatu alitoa rambirambi zake kwa familia za waliofariki.
Wizara ya mambo ya ndani ilisema kuwa wafanyakazi wazima moto 7,500 na malori 350 ya zima moto yanatumiwa yakisaidiwa na ndege ili kukabiliana na moto huo.
Forum