Kampuni ya kutengeneza chanjo ya Covid-19 inaishitaki kampuni mshindani ya Pfizer na ile ya Ujerumani BioNTech, ikiishutumu kwa kuiga teknolojia ya Moderna ili kutengeneza chanjo zake zenyewe.
Moderna Ijumaa imeeleza chanjo za Pfizer na BioNTech zimekiuka ubunifu ulio andikishwa na Moderna miaka kadhaa ya nyuma ikilinda teknolojia iliyotumika katika chanjo yake ya Spikevax.
Kampuni hiyo imefungua mashitaka ya ukiukwaji wa ubunifu katika mahakama ya juu ya Marekani na Ujerumani.
Msemaji wa Pfizer Pam Eisele amekataa kuzungumza chochote kuhusiana na hilo akisema kampuni yao haijapata nakala ya mashitaka yaliyofunguliwa.