Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:23

Moderna kujenga kiwanda cha kwanza cha kutengeneza chanjo ya Covid barani Afrika


Chupa la Chanjo ya Covid 19 ya Moderna ikionyeshwa kwenye duka la dawa Portland Oregon hapa Marekani. Disemba 27,2021. Picha ya AP
Chupa la Chanjo ya Covid 19 ya Moderna ikionyeshwa kwenye duka la dawa Portland Oregon hapa Marekani. Disemba 27,2021. Picha ya AP

Kampuni ya Marekani ya kutengeneza chanjo Moderna, imesema leo Jumatatu kwamba itajenga kiwanda cha kwanza cha kutengeneza chanjo barani Afrika, baada ya kusaini mkataba na serikali ya Kenya.

Kiwanda hicho kitatengeneza dozi milioni 500 za Covid 19 mwaka huu.

Kampuni hiyo inatarajiwa kuwekeza dola milioni 500 katika kiwanda hicho kipya ambacho kitatengeneza chanjo kwa ajili ya wakazi bilioni 1.3 wa bara la Afrika, ambalo raia wake wengi sana hawakupata chanjo za Covid.

“Kupambana na janga la Covid 19 katika miaka miwili iliyopita ilitukumbusha kazi ambayo lazima ifanywe ili kuhakikisha usawa wa afya ulimwenguni. Moderna ina dhamira ya kuwa sehemu ya suluhisho”, mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo, Stephane Bancel amesema katika taarifa.

Moderna imesema inatumai kutumia kiwanda hicho kugawa dozi za chanjo ya Covid 19 kwa mataifa ya Afrika ifikapo mapema mwaka ujao.

Nae rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema “ Uwekezaji wa Moderna nchini Kenya utasaidia kuendeleza upatikanaji sawa wa chanjo kote duniani na ni ishara ya maendeleo ya kimuundo ambayo yatawezesha Afrika kuwa kichocheo cha ukuaji endelevu wa kiuchumi ulimwenguni”.

XS
SM
MD
LG