Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:06

Mnangagwa na Chamisa wamefanya kampeni za mwisho Zimbabwe


Emerson Mnangagwa akiwa katika kampeni za mwisho mwisho
Emerson Mnangagwa akiwa katika kampeni za mwisho mwisho

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa wamefanya kampeni zao za mwisho-mwisho kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo siku ya Jumatatu wakiwa na nia ya kuondoa miongo kadhaa iliyopita ya kudorora kwa uchumi na siasa za chama kimoja.

Upigaji kura huo utakuwa wa kwanza bila ya kulihusisha jina la kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kwenye sanduku la kupiga kura baada ya kujiuzulu Novemba mwaka jana kufuatia hatua ya jeshi kuchukua madaraka na shinikizo kutoka chama tawala cha ZANU-PF ambacho kilikuwa kikimuunga mkono kiongozi huyo.

Takribani wapigakura milioni tano wa Zimbabwe walikulia chini ya utawala wa Mugabe uliodumu kwa miaka 37. Wafuasi wa Mnangagwa mwenye miaka 75, aliyekuwa naibu wa zamani wa Mugabe, pamoja na kiongozi wa upinzani wa chama cha Movement for Democratic Change-MDC, Chamisa mwenye miaka 40 walikusanyika katika matukio tofauti mjini Harare siku ya Jumamosi.

Nelson Chamisa wa MDC akizungumza na wafuasi wake kwenye kampeni
Nelson Chamisa wa MDC akizungumza na wafuasi wake kwenye kampeni

Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press siku ya Ijumaa, Chamisa aliishutumu tume ya uchaguzi Zimbabwe haipo sahihi inampendelea Mnangagwa, madai ambayo Rais Mnangagwa pamoja na tume hiyo ya uchaguzi wanayapinga. Chamisa aliapa kufanya maandamano ya amani kama uchaguzi hautakuwa wa haki.

XS
SM
MD
LG