Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 03:05

Mmarekani aliyekuwa anashikiliwa Russia aachiwa huru na kurejea nyumbani


Rais Donald Trump, akiwa pamoja na Marc Fogel, akizungumza katika Chumba cha mapokezi ya wanadiplomasia White House, Februari 11, 2025.
Rais Donald Trump, akiwa pamoja na Marc Fogel, akizungumza katika Chumba cha mapokezi ya wanadiplomasia White House, Februari 11, 2025.

Marc Fogel, mwalimu raia wa Marekani ambaye alikuwa anazuiliwa nchini Russia tangu Agosti 2021 kwa kuleta bangi inayoruhusiwa na madaktari nchini humo, aliachiliwa na Moscow Jumanne na alirejea nyumbani, White House ilitangaza.

Mwalimu huyo wa Historia mwenye umri wa miaka 63, ambaye alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 14, alitarajiwa kuungana na familia yake katika jimbo la mashariki la Pennsylvania Jumanne jioni.

Aliondoka kwenye anga ya Russia akiwa ndani ya ndege binafsi ya Steve Wikoff, mjumbe wa Rais Donald Trump wa masuala ya kigeni ambaye alisaidia katika majadiliano ya kuachiliwa kwake.

Marc Fogel Jumanne Jioni alipokelewa White House na Rais Donald Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG