Mashahidi nchini somalia wanasema mlipuko mkubwa umetokea karibu na eneo linaloshikiliwa na wanamgambo wa al- shabab nje ya mji mkuu wa somalia.
Mashahidi wanasema mlipuko huo ulitokea jumapili karibu na Afgoye takriban kilomita 30 kutoka Mogadishu.
Wanaeleza kuwa waliona mwanga katika mawingu ukifuatia na mlipuko mkubwa.
Jeshi la Kenya lilitishia kufanya shambulizi la anga katika maeneo ya
waasi nchini somalia lakini halikueleza haraka juu ya mlipuko huo.
Msemaji wa jeshi la Kenya alisema mapigano baina ya wanajeshi wa Kenya na wanamgambo wa al- shabab kusini mwa somalia jumamosi jioni yameuwa waasi tisa na kujerihi wanajeshi wanne.