Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:55

Mlipuko kwenye bomba la mafuta waua watu 12 kusini mwa Nigeria


katika picha hii iliyonaswa kwa video, moto wanaonekana baada ya mlipuko kwenye bomba la mafuta huko Nembe, Nigeria, Machi 1, 2019.
katika picha hii iliyonaswa kwa video, moto wanaonekana baada ya mlipuko kwenye bomba la mafuta huko Nembe, Nigeria, Machi 1, 2019.

Mlipuko kwenye bomba la mafuta ghafi Ijumaa, kusini mwa Nigeria, umewaua watu 12 waliokuwa wanaiba mafuta, polisi wamesema.

Polisi wa jimbo la Rivers wamesema mlipuko katika wilaya ya Emuoha ulisababishwa na wezi na waharibifu.

“Waathiriwa walikuwa wakichota mafuta ghafi wakati bomba hilo liliposhika moto,” msemaji wa polisi wa jimbo Grace Iringe-Koko amesema katika taarifa.

Amesema watu 12 wanaaminika wamechomwa moto hadi kufa.

Msemaji huyo wa polisi amewaonya watu dhidi ya uharibifu wa mabomba na wizi wa mafuta ambalo ni jambo la kawaida katika jimbo hilo, vitendo ambavyo vinaathiri uzalishaji wa mafuta na mapato ya taifa.

XS
SM
MD
LG