Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 04:23

Mkutano wa siku tatu wa ASEAN wanza Alhamisi nchini Laos


Waziri wa mambo ya kigeni wa Laos, Saleumxay Kommasith (katikati) akizungmza kwenye mkutano wa 57 wa (ASEAN) mjini,Vientiane. Julai 25, 2024.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Laos, Saleumxay Kommasith (katikati) akizungmza kwenye mkutano wa 57 wa (ASEAN) mjini,Vientiane. Julai 25, 2024.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Asia Kusini Mashariki, pamoja na wanadiplomasia wa juu kutoka washirika muhimu ikiwemo Marekani na China wanakutana kwenye mji mkuu wa Laos, Alhamisi, kwenye kikao cha ASEAN.

Mazungumzo yao yanalenga kuangazia kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Myanmar, na kuongezeka kwa mivutano kwenye bahari ya South China Sea, miongoni mwa masuala mengine ya kikanda.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja pembeni mwa mkutano huo mjini Vientiane, unaofanyika wakati Beijing, na Washington, wakijitahidi kuongeza ushawishi wao kwenye eneo hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Laos, Saleumxay Kommasith amewashukuru wanachama wa ASEAN, pamoja na washirika wao, kwa juhudi zao za pamoja ambazo zimepelekea hatua zilizopigwa, huku akisisitiza umuhimu wa kundi hilo wa kuzingatia amani na uthabiti.

Kwa mataifa wanachama wa ASEAN, Indonesia, Thailand, Singapore, Ufilipino, Vietnam, Malaysia, Myanmar, Cambodia, Brunei na Laos, suala la ghasia za Myanmar ni kipaumbele cha mazungumzo yao.

Forum

XS
SM
MD
LG