Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:57

Mkutano wa G7 waanza nchini Japan huku Russia ikilengwa kwa vikwazo vipya


Mkutano wa 49 wa mataifa tajiri zaii duniani G7 mjini Hiroshima, Japan.
Mkutano wa 49 wa mataifa tajiri zaii duniani G7 mjini Hiroshima, Japan.

Viongozi wa G- 7 wanakutana Japan  mwishoni mwa wiki wakiwa na mawazo ya kuiwekea Russia vikwazo vipya.

Madini ya chuma yenye faida kubwa sana yanalengwa, na huenda Almasi nayo pia inaweza kulengwa katika vikwazo.

Maafisa wa G-7 wamesema hakutakuwa na makubaliano yatakayofikiwa mwishoni mwa wiki, lakini suala la almasi huenda litakuwa katika waraka wa mwisho wa mkutnao huo wa viongozi.

Wazo la kuzuia biashara hiyo lilitolewa na Poland mwezi Aprili. Lakini hatua yoyote kama hiyo inaweza kuvurugwa na mjadala wenye mkanganyiko ndani ya EU.

Mataifa mengine ya G- 7 yana wasiwasi kuwa vikwazo vinaweza kushuhudia biashara ikifanywa kupitia nchi kama india badala yake.

Vyanzo viwili katika kundi hilo vimesema wazo lilikuwa kuendeleza teknolojia za ufuatiliaji ambazo zinaweza kuzuiya hilo lakini hatua hiyo inaweza kuchukua muda.

Licha ya hayo, rais wa baraza la ulaya Charles Michel amesema EU itaweka vikwazo.

Uingereza kwa upande wake haitaki kusubiri, waziri mkuu Rishi Sunak anatarajiwa kutangaza kupiga marufuku almasi na vyuma ikiwemo na shaba na nickel kutoka Russia.

shinikizo zaidi la kuiwekea vikwazo Russia litaongezeka mwishoni mwa wiki pale Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky atakapokwenda Hiroshima kwenye Mkutano huo.

XS
SM
MD
LG