Waziri wa mambo ya nje wa India, S. Jaishankar aliwaambia wanahabari kuwa mgawanyiko ulilizuia kundi hilo kuwa na taarifa ya pamoja, na kuelezea maoni tofauti sana ya baadhi ya nchi kuhusiana na mzozo huo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya nje wa Russia, Sergey Lavrov, na mwenzao wa China, Qin Gang, ni miongoni mwa wale ambao walikuwepo New Delhi.
Afisa mwandamizi wa Marekani aliwaambia wanahabari kwamba Blinken alikutana na Lavrov pembeni ya mkutano huo wa Alhamisi, na kusisitiza kwamba Marekani iko tayari kuiunga mkono Ukraine, kujitetea katika mzozo huu ambazo umekuwa na uharibifu mkubwa.