Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 06, 2025 Local time: 15:49

Mkutano kuhusu Somalia wafanyika London


Mkutano kuhusu hali ya Somalia wafanyika mjini London Alhamisi, tarehe 11, Mei, 2017.
Mkutano kuhusu hali ya Somalia wafanyika mjini London Alhamisi, tarehe 11, Mei, 2017.

Mkutano wa kutathmini hali ya usalama na athari zilizoletwa na majanga katika nchi ya Somalia ulifanyika mjini London siku ya Alhamisi na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo katibu mkuu wa umoja wa mataifa, marais na viongozi wa serikali kadhaa.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres na rais wa Somalia Mohamed Abdulahi Farmajo walikuwa wenyekiti wa kikao hicho, kilichojadili mikakati iliyowekwa na inayofaa kuwekwa ili kuimarisha usalama na siasa za nchi hiyo iliyokumbwa na mizozo kwa miaka mingi.

Marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Uganda, Yoweri Museveni walikuwa baadhi ya viongozi kutoka Afrika waliohudhuria kongamano hilo.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza ilisema kuwa nchi hiyo iko tayari kuanza ushirikiano mpya na Somalia.

Wakati wa mkutano huo, rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed aliwaomba viongozi wa nchi zenye nguvu duniani kumsaidia kupambana na maadui wa ugaidi, rushwa na umaskini.

Mkutano huo wa kimataifa unalenga kudumisha uthabiti chini ya uongozi mpya katika nchi iliyoharibiwa kwa vita.

Rais Mohamed aliuambia mkutano huo kwamba nchi yake inaweza kustawi kutokana na utamaduni wa kawaida wa wasomali kufanya biashara ikiwa vitisho vya nja, uharamia na ugaidi vitasitishwa.

Mkutano huo wa siku moja aidha ulidhamiria kufikia mkataba mpya kati ya Somalia na mtandao wa mataifa yanayoisaidia ili kuharakisha mafanikio katika usalama, maendeleo na uchumi ifikapo mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG