Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:31

Mkataba wa Nyuklia: Rouhani asema Marekani itajutia uamuzi wake


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Iran amesema Jumapili iwapo Marekani itajiondoa katika makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa na Iran na mataifa makubwa duniani ijue kuwa Washington itakuja kujutia uamuzi wake huo.

Hassan Rouhani amesema katika hotuba yake kupitia televisheni, “ Iwapo Marekani itaamua kujiondoa katika mkataba huo wa nyuklia, hivi karibuni tu mtaona kuwa watakuwa na majuto kuliko wakati wowote katika historia.

“Tunao mpango wa kupinga uamuzi wowote ule utakaochukuliwa na Trump dhidi ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkataba huo,” Rouhani amesema katika hotuba yake iliyotangazwa moja kwa moja na televisheni ya taifa, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

“Amri imetolewa kwa taasisi yetu ya nguvu za atomic… na kwa sekta ya uchumi kukabiliana na njama za Marekani dhidi ya nchi yetu,” Rouhani amesema hilo katika mkutano wa hadhara huko upande wa kaskazini mashariki mwa Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ifikapo Mei 12 atafanya uamuzi iwapo Washington ibakie kuwa mshiriki wa mkataba huo wa nyuklia.

Amesema kuwa atajiondoa katika mkataba huo iwapo hautafanyiwa marekebisho, likiwemo pendekezo la kuidhibiti programu ya kombora la ballistika ya Iran, ambayo Iran imeendelea kusisitiza kuwa ni kinga yake katika kujihami.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema Alhamisi Iran haitorejea kufanya mazungumzo kujadili mkataba wa nyuklia wa 2015 uliofikiwa na mataifa makubwa duniani.

XS
SM
MD
LG