Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:24

Atakayefuja fedha za jimbo jela miaka mitano


Ramani ya Tanzania.
Ramani ya Tanzania.

Serikali ya Tanzania imesema fedha zote za mfuko wa jimbo zimeshawasilishwa na imewataka wabunge ambao hawajapata fedha hizo kufuatilia katika matawi ya benki zao nchini humo.

Serikali ya Tanzania imesema fedha zote za mfuko wa jimbo zimeshawasilishwa na imewataka wabunge ambao hawajapata fedha hizo kufuatilia katika matawi ya benki zao nchini humo.

Naibu waziri wa fedha wa Tanzania Omar Yusufu mzee akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA, amesema malalamiko yaliyokuwa yanatolewa na wabunge hao dhidi ya serikali kuhusu fedha hizo hayana msingi.
Waziri huyo amesema fedha hizo zimechelewa kufika katika jimbo la Zanzibar kwa sababu za mawasiliano ya benki ambapo itachukua siku 14 pesa hizo kufika katika majimbo yao.

Akijibu swali kama fedha hizo hazitatumiwa na wabunge kufanyia kampeni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu naibu waziri huyo amesema itakuwa ni kinyume cha sheria na endapo mbunge ama mtu mwingine yeyote atazitumia fedha hizo kinyume na malengo atafungwa miaka mitano jela ama kulipa faini ya shilingi milioni kumi za Tanzania.

Amesema mgawanyo wa fedha hizo ni kuanzia milioni 80,50 hadi 25 kutegemea na ukumbwa wa jimbo.
Akizungumzia fedha hizo mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema upo uwezekano mkubwa kwa wabunge kuzitumia fedha hizo kufanyia kampeni ili iwe rahisi kwao kushinda katika uchaguzi ujao.

Amesema udhibiti wa fedha hizo ungekuwa na tija kama zingepelekwa katika fungu la halmashauri za wilaya badala ya mfuko wa jimbo ambao mwenyekiti wake ni mbunge na ndiye anayeunda kamati ya namna ya kuzitumia fedha hizo.

XS
SM
MD
LG