Mikataba hiyo inahusiana na miundombinu, huduma za usafirishaji wa bidhaa, usimamizi wa bandari, kilimo cha chakula, viwanda vya dawa, mafuta ambayo hayajasafishwa na nishati mbadala, na usalama wa mitandao, na thamani yake ilikuwa dola bilioni 7.7, gazeti la Misri la Al Ahram limesema.
“Mikataba 14 ya uwekezaji yenye thamani ya dola bilioni 7.7 ilisainiwa kati ya kampuni kubwa za Saudia zinazofanya shughuli tofauti za kiuchumi na kampuni kadhaa za Misri na maafisa, shirika la habari la serikali ya Saudia Al-Ekhbaria limesema kwenye Twitter.
Wizara ya uwekezaji ya Saudia imesema mikataba hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Biashara kati ya Misri na taifa hilo la kifalme iliongezeka kwa zaidi ya asilimia 62 mwaka jana ikilinganishwa na mwaka wa 2020, na kufikia dola bilioni 9.1, kulingana na takwimu rasmi za Misri.